Imeelezwa
kuwa msanii huyu, alianza safari yake ya kuelekea umauti wakati akiwa
katika harakati za kurekodi filam, ambapo alianza kujisikia vibaya na
kupelekwa katika Hospitali ya Mwananyamala, ambako alipatiwa matibabu ya
awali na kulazimika kufanyiwa upasuaji ambao kusababisha kuhamishiwa
Hospitali ya Muhimbili. Kilisema chanzo cha habari hizi.
JOHN STEPHANO- Enzi ya uhai wake
Kwa mujibu wa taarifa kutoka kwa viongozi wa Wasanii zinasema kuwa Mipango ya mazishi inafanyika Nyumbani kwao Mwananyamala 'A' jirani na Kopakabana Bar jijini Dar es Salaam. Marehemu John anaetarajiwa kuzikwa leo jumanne katika Makaburi ya Kinondoni Dar es Salaam.
*MWILI WA MSANII JOHN MAGANGA WAAGWA LEO JIJINI DAR ES SALAAM
Wasanii
wa Bongo Movie wakibeba jeneza lenye mwili wa msanii mwenzao, John
Maganga, wakati wa kuaga mwili wa msanii huyo, Mwananyamala, Dar es
Salaam. Maganga amefariki dunia Jumamosi ya wiki iliyopita, katika
hospitali ya Muhimbili, jijini Dar es Salaam, baada ya kuugua ghafla. John amezikwa leo katika Makaburi ya Kinondoni.
*MSANII WA KAOLE, MLOPELO AFARIKI DUNI, KUZIKWA LEO TMK
MSANII
aliyepata umaarufu mkubwa enzi za Kaole ya ITV, Mlopelo, amefariki
dunia jana mchana, kwenye hospitali ya Temeke, jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu
wa msemaji wa familia aliyejitambulisha kwa jina moja la Azizi,
aliyeongea na tovuti ya Saluti5.com jana usiku, ni kwamba katika maisha
yake yote, Mlopelo alikuwa anasumbuliwa na maumivu ya mwili yaliyokuwa
yakitulia na kuibuka tena hadi umauti ulipomfika.
Aziz, amesema mazishi yalipangwa kufanyika Temeke leo Ijumaa saa 4 na kwamba msiba uko Temeke Wailes mtaa wa Boko.
No comments:
Post a Comment