TIMU ya Coastal
Union ya Tanga imeanza vizuri michuano ya kuwania Kombe la Uhai inayoshirikisha
wachezaji wenye umri chini ya miaka 20 wa klabu za Ligi Kuu ya Vodacom baada ya
kuifunga Tanzania Prisons mabao 2-1.
Mechi hiyo
ya kundi A imechezwa leo asubuhi (Desemba 11 mwaka huu) Uwanja wa Kumbukumbu ya
Karume, Dar es Salaam. Coastal Union ilimaliza kipindi cha kwanza ikiwa tayari
imepachika mabao hayo yaliyofungwa dakika ya 24 na 33 kupitia kwa Ramadhan Same
na Yusuf Chuma.
Tanzania
Prisons ambayo itacheza mechi yake pili kesho jioni (Desemba 12 mwaka huu)
Uwanja wa Azam ulioko Chamazi dhidi ya JKT Ruvu ilipata bao lake dakika moja
kabla ya filimbi ya mwisho.
Mechi
nyingine za kesho ni Toto Africans dhidi ya Coastal Union itakayochezwa saa 2
asubuhi Uwanja wa Azam. Katika kundi B, Simba na African Lyon zitaoneshana kazi
asubuhi Uwanja wa Karume wakati Azam na Polisi Morogoro zitacheza saa 10 jioni
kwenye uwanja huo huo.
Kundi C
kesho ni Kagera Sugar vs Oljoro JKT saa 2 asubuhi Uwanja wa Karume, na Yanga na
Ruvu Shooting zitaumana saa 10 jioni kwenye Uwanja wa Azam.
No comments:
Post a Comment