Saturday, December 29, 2012

BONGE LA KITASA LA ZAMBIA NA TP MAZEMBE

STOPPILA Sunzu anaaminika kuwa miongoni mwa mabeki bora barani Afrika kutokana na mchango wake kwa mafanikio ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na timu ya Taifa ya Zambia, Chipolopolo. 

 "Nakwenda kuchezea Reading na nategemea kuondoka Zambia kwenda Uingereza baada ya siku chache na nikifika huko nitakwenda kukamilisha mkataba," anaeleza Stoppila.

Stoppila, hata hivyo, mara ya kwanza alitajwa kuwa anakwenda kujiunga na Arsenal ingawa amekwama baada ya klabu hiyo kutaka kumfanyia majaribio.

"Sitaenda kucheza Arsenal kwa sababu wanataka kuniona nikicheza mechi zaidi. Kocha Arsene Wenger anataka kuona uchezaji wangu.

"Ninategemea mambo yatakwenda vizuri Reading ingawa kwa sasa akili yangu ni kuisaidia Zambia kuibuka kidedea huko Afrika Kusini,"anasema Sunzu.

Sunzu anaeleza amefurahia nafasi ya kwenda kucheza England kwani malengo yake mara zote yamekuwa kucheza Ulaya.

"Hii ni nafasi muhimu katika maisha yangu ya soka. Nitajituma ili kila kitu kiende sawa." 


 STOPPILA FELIX SUNZU
Amezaliwa: Juni 22, 1989
Mahali: Ndola, Zambia
Urefu: Ft 6 na inchi 3
Nafasi: beki ya kati na kiungo mkabaji
Klabu: Konkola Blades 2005�2008,
Zanaco 2008�2009,
LB Chateauroux 2008�2009,
TP Mazembe 2009�
Taifa: Zambia

No comments:

Post a Comment