TIMU ya Mtibwa
Sugar ya Morogoro leo asubuhi (Desemba 14 mwaka huu) imeibuka na ushindi wa
mabao 3-1 dhidi ya Toto Africans ya Mwanza katika mechi ya michuano ya Kombe la
Uhai inayoshirikisha timu za vijana wenye umri chini ya miaka 20 (U20) za klabu
za Ligi Kuu ya Vodacom.
Juma Luzio
alifunga mabao yote matatu (hat trick) katika mechi hiyo iliyochezwa Uwanja wa
Kumbukumbu ya Karume jijini Dar es Salaam. Alifunga mabao hayo dakika za 44,81
na 88.
Hata hivyo,
Toto Africans ndiyo walioanza kufunga katika mechi hiyo ya kundi A. Bao hilo
katika michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa kupitia
maji Uhai lilifungwa dakjika ya 22 na Pastol Makula.
Nayo Simba
imenguruma baada ya kuitandika Mgambo Shooting ya Tanga katika mechi nyingine
ya michuano hiyo iliyochezwa leo asubuhi kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi.
Wafungaji kwa washindi walikuwa Ramadhan Mdoe dakika ya 19, Mohamed Salum
dakika ya 77 na Ramadhan Singano dakika ya 89.
Michuano
hiyo inaendelea leo mchana na jioni. Mechi ya Ruvu Shooting na Kagera Sugar
iliyokuwa ichezwe mchana Uwanja wa Azam, Chamazi sasa itafanyika saa 10 kamili
jioni katika Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Mechi nyingine
za leo ni Coastal Union vs JKT Ruvu (mchana- Karume), African Lyon vs Azam
(jioni- Chamazi). Vilevile mechi kati ya JKT Oljoro na Yanga inachezwa leo
Uwanja wa Chamazi.
Kesho
(Desemba 15 mwaka huu) ni mapumziko, na michuano hiyo itaendelea Jumapili
kwenye viwanja vyote viwili- Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume na Uwanja wa Azam-
Chamazi.
............................................................................MWISHO..................................................................
WAWAKILISHI
wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho la Soka Afrika, (CAF), Azam FC
wanaondoka mchana wa leo kwenda Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kucheza
mashindano ya Kombe la Hisani.
Michuano
hiyo inatarajiwa kuanza leo na itafikia tamati Desemba 23, mwaka huu na Azam FC
itashiriki kwa lengo la kuwapa mazoezi na uzoefu wachezaji wake kabla ya
kuingia kwenye Kombe la Shirikisho mwakani.
Azam pia,
itatumia mashindano hayo kama fursa ya kuwapima wachezaji wake kabla ya kuanza
kwa Kombe la Shirikisho mwakani, ambako wamepangwa kuanza na Al Nasr Juba ya
Sudan Kusini.
Hata hivyo,
katika kikosi cha Azam kitakachoondoka leo, hawamo wachezaji wake wapya wa
kigeni, iliyowasajili beki Mkenya, Joackins Atudo na mshambuliaji Mganda, Brian
Umony.
Mashindano
hayo yatashirikisha timu kubwa za kutoka Kongo kama DC Motema Pembe na A.S.
Vita Club, wakati timu kutoka nje ya Kongo mbali na Azam FC, kuna Tusker FC ya
Kenya, Gombe United ya Nigeria na Diable Noirs ya Kongo Brazzaville.
Kikosi cha
Azam kinachokwenda DRC ni; Mwadini Ally, Jackson Wandwi, Gaudence Mwaikimba,
Himidi Mao, Ibrahim Mwaipopo, Jabir Aziz, Kipre Tchetche, Kipre Balou, Luckson
Kakolaki, Samir Hajji Nuhu, Zahoro Pazi, Seif Abdallah, Malika Ndeule, Omar Mtaki,
Abdi Kassim, Uhuru Suleiman na David Mwantika.
Wachezaji wengine
ambao hawahusiki katika safari hiyo, ni wale waliopo kwenye kikosi cha timu ya
taifa, Khamis Mcha ‘Vialli’, John Bocco ‘Adebayor’ na Salum Abubakar, wakati
wengine ni waliosimamishwa kwa tuhuma za kuhujumu timu, Aggrey Morris, Deo Munishi ‘Dida’, Erasto Nyoni ambao wote wapo
timu ya taifa pia na Said Mourad.
Kikosi
hicho kitaongozwa na kocha Mkuu, Muingereza Stewart Hall.
......................................................................MWISHO................................................................................
KIKOSI BORA CHA TIMU YADUNIA |
No comments:
Post a Comment