Monday, December 10, 2012

TAIFA STARS HAPO SASA SELEMBE NJE

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mdenmark, Kim Poulsen ametaja kikosi cha 
wachezaji 24, ndani yake akiwatema chipukizi aliokuwa akiwakomaza kwenye timu hiyo, Ramadhani Singano ‘Messi’ na Edward Christopher, wote wa SImba SC.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo ofisi za Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Poulsen alisema kikosi hicho kitaingia kambini keshokutwa kwa ajili ya kujiandaa na mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya mabingwa wa Afrika, Zambia, Chipolopolo itakayochezwa Desemba 22, mwaka huu Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mbali na Cannavaro na Aishi Mangula, nyota wengine wapya walioitwa katika kikosi hicho ni pamoja na Hamisi Mcha ‘Vialli’ na Samir Hajji Nuhu wote wa Azam FC.
Wengine walioitwa ni makipa; Juma Kaseja (Simba) na Mwadini Ally (Azam FC), mabeki; Amir Maftah (Simba), Shomari Kapombe (Simba), Erasto Nyoni (Azam), Nasoro Masoud ‘Chollo’ (Simba) na Aggrey Morris wa Azam FC.
Viungo ni Mwinyi Kazimoto (Simba), Mrisho Ngassa (Simba), Frank Domayo (Yanga), Amri Kiemba (Simba), Athumani Idd ‘Chuji’ (Yanga), Shaaban Nditi (Mtibwa Sugar), wakati washambuliaji ni Mbwana Samatta, Thomas Ulimwengu (TP Mazembe, DRC), John Bocco (Azam), Simon Msuva (Yanga).
 
 KIKOSI CHA MAUAJI MABINGWA WA AFRIKA ZAMBIA
 
KOCHA Mkuu wa timu ya Zambia, Chipolopolo, ambayo ni mabingwa wa Afrika, Herve Renard ametaja kikosi cha wachezaji 24 kitakachoikabili Taifa Stars kwenye mechi ya kirafiki itakayochezwa Desemba 22 mwaka huu jijini Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa Chama cha Soka Zambia (FAZ), wachezaji hao ni Chintu Kampamba, Chisamba Lungu, Christopher Katongo, Danny Munyau, Davy Kaumbwa, Derrick Mwansa, Evans Kangwa, Felix Katongo na Francis Kasonde.
Wengine ni Given Singuluma, Hichani Himonde, Isaac Chansa, James Chamanga, Jimmy Chisenga, Jonas Sakuwaha, Joshua Titima, Kalililo Kakonje, Moses Phiri, Mukuka Mulenga, Rainford Kalaba, Rodrick Kabwe, Salulani Phiri, Shadrack Malambo na Stoppila Sunzu.
 

No comments:

Post a Comment