uwanja wa ndege uturuki
Na Prince Akbar
YANGA SC, wanatarajiwa
kuanza mazoezi leo katika viwanja vya hoteli ya Fame mjini Antalya, Uturuki, baada
ya kuwasili jana majira ya saa 10:30 jioni, kwa saa za Afrika Mashariki.
Mabingwa
mara tano wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, Kombe la Kagame, wapo
nchini humo kwa uenyeji wa kampuni ya Utalii ya Team Travel ya nchini humo na
watakuwa huko kwa wiki mbili kuanzia jana.
Vinara hao
wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, wamefikia katika hoteli ya Fame Residence
Lara & Spa kilomita chahce kutoka katika Uwanja wa ndege wa Antalya, ambako
hoteli ya Fame Residence ipo mwambaoni mwa bahari ya Mediteranian.
Yanga iliondoka
Dar es Salaam Alfajiri ya jana, saa 10:30 na kikosi kizima pamoja na benchi la
ufundi kamili.
Waliopo
Uturuki ni makipa; Ally Mustafa 'Barthez', Said Mohamed na Yussuf Abdul, mabeki
Juma Abdul, Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Stefano Mwasyika, Oscar Joshua, Mbuyu
Twite, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Ladisalus Mbogo na Kelvin Yondani.
Viungo ni Athumani
Iddi ‘Chuji’, Frank Domayo, Haruna Niyonzima, Kabange Twite, Nurdin Bakari, Omega
Seme, Simon Msuva, Rehani Kibingu, Nizar Khalfani na David Luhende wakati washambuliaji
ni Didier Kavumbagu, Said Bahanunzi, Jerry Tegete, George Banda na Hamisi Kiiza.
Upande wa
benchi la ufundi ni Kocha Mkuu Mholanzi, Ernie Brandts, Kocha Msaidizi Freddy
Felix Minziro na Kocha wa makipa, Razak Ssiwa, na Maofisa wengine ni Daktari wa
timu, Sufiani Juma, Meneja Hafidh Saleh, Ofisa Habari, Baraka Kizuguto Mjumbe
wa Kamati ya Utendaji, Mohammed Nyenge.
Mwandishi wa
Gazeti la Mwanaspoti, Michael Momburi aliondoka jana usiku, yeye akigharamiwa
na kampuni yake.
Ziara ya
mwisho katika nchi ya maana kwa Yanga, ilikuwa mwaka 2008 nchini Afrika Kusini,
ambako iliweka kambi ya zaidi ya wiki mbili wakati huo ikiwa chini ya Profesa
Dusan Savo Kondic, raia wa Serbia.
Zaidi ya
hapo, mwaka huu Yanga ilikwenda Kigali, Rwanda kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya
Bara, kwa mwaliko wa rais wa nchi hiyo, Paul Kagame. Yanga pia imewahi kufanya ziara Brazil mwaka
1974 na Romania 1979.
Yanga SC ni
klabu kongwe Tanzania ambayo kati ya zinazoshiriki Ligi Kuu kwa sasa, yenyewe
ndio yenye umri mkubwa zaidi.
Ingawa
historia inasema Yanga ilizaliwa mwaka 1935 na Simba mwaka 1936, lakini ukizama
ndani utagundua kwamba, huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa utani na upinzani wa jadi,
baina ya miamba hiyo ya soka nchini.
Kulikuwa
kuna timu inaitwa New Youngs, ambayo mwaka 1938 ilisambaratika na baadhi ya
wachezaji wake wakaenda kuunda timu iliyokuwa ikiitwa Sunderland, ambayo hivi
sasa inajulikana kama Simba.
Kabla ya
kutokea vurugu zilizoisambaratisha New Youngs, vijana wa Dar es Salaam walikuwa
wana desturi ya kukutana viwanja vya Jangwani kufanya mazoezi na baada ya muda
wakaamua kuunda timu yao, waliyoipachika jina Jangwani.
Ndani ya
kipindi kifupi tu, timu hiyo iliteka hisia za wengi, waliojitokeza
kujiandikisha uanachama wa klabu hiyo. Miongoni mwa waliovutika na uanachama wa
klabu hiyo ni Tarbu Mangara (sasa marehemu) na ilipofika mwaka 1926, walifanya
mkutano wa kwanza katika eneo ambalo hivi kuna shule ya sekondari ya Tambaza.
Miongoni mwa
yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni kuiboresha timu hiyo, ambayo wachezaji
wake wengi walikuwa wafanyakazi wa Bandarini na mashabiki wake wengi walikuwa
wabeba mizigo wa bandarini.
Baada ya
mkutano huo, timu hiyo ilibadilishwa jina na kuwa Navigation, iliyotokea kuwa
moto wa kuotea mbali katika timu za Waafrika enzi hizo, kabla ya uhuru wa
Tanganyika. Timu kama Kisutu, Kitumbini, Gerezani na Mtendeni zilikuwa hazifui
dafu kwa wana Jangwani hao.
Ikiwa
inatamba kwa jina la Navigation, wanachama wa timu hiyo walikuwa wakitembea
kifua mbele na kuwatambia wapinzani, kwamba wao ndiyo zaidi. Kwa sababu katika
kipindi hicho, Italia ilikuwa inatamba kwenye ulimwengu wa soka, wanachama wa
timu hiyo nao waliamua kuibadilisha jina timu yao na kuiita Taliana.
Taliana
ilipata mafanikio ya haraka na haikushangaza ilipopanda hadi Ligi Daraja la
Pili Kanda ya Dar es Salaam, mwanzoni mwa miaka ya 1930. jina la Taliana
waliamua kuachana nalo mapema, kabla ya kuingia kwenye ligi hiyo, hivyo
wakaanza kujiita New Youngs.
Lakini kila
ilipokuwa ikibadilisha jina, ilikuwa ikifanya vitu pia, kwani wakiwa na jina la
New Youngs, waliweza kutwaa Kombe la Kassum, lililoshirikisha timu mbalimbali
za Dar es Salaam.
Hatimaye
ukawadia mwaka mbay
a kwa New Youngs, 1938 wakati baadhi ya wachezaji
walipojitoa na kwenda kuanzisha Sunderland. Kwa sababu hiyo, waliobaki wakaamua
kubadili jina na kuwa Young Africans, jina ambalo mashabiki wake wengi
walishindwa kulitamka vizuri hivyo kujikuta wakisema Yanga. Safari njema Yanga
SC.
..................................................................................................................................................................