Friday, January 4, 2013

MSIBA WA SAJUKI KATIKA PICHA

VIONGOZI WA SERIKALI WAKIWASILI: Mbunge wa jimbo la Segerea, Dar es Salaam, ambaye pia ni Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk. Makongoro Mahanga (wa tatu kushoto) akiwa ameambatana na Mbunge wa jimbo la  Kinondoni Mh.Iddi Azzan wakipokelewa na Rais wa Shirikisho la Filamu nchini (TAFF) Bw. Simon Mwakifamba na wasanii wengine wa filamu baada ya kuwasili nyumbani kwa Marehemu Sajuki kwa ajili ya kuhani msiba huo.
Katibu wa Fedha msibani hapo mchekeshaji maarufu Steve Nyerere akiwakaribisha waheshimiwa wabunge kuzungumza na hadhira ya waombolezaji (hawapo pichani
Mkuu wa Itifaki msibani hapo Bw. Simon Simalenga wa Clouds Media akimpokea  Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete alipowasili nyumbani kwa marehemu Sajuki kwa ajili ya kuhani maeneo ya Tabata Bima jijini Dar es Salaam.
Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya wasanii wa filamu wakisikiliza nasaha za Bw. Ridhiwani Kikwete (hayupo pichani).
Mwenyekiti wa kamati ya Kusaidia timu ya Taifa ya Vijana Serengeti Boys Bw. Ridhiwani Kikwete akizungumzia marehemu Sajuki na kuwataka wanawake kuiga mfano wa Maisha ya Sajuki na Wastara jinsi walivyokuwa wakiishi na Upendo mpaka Umauti ulipomkuta marehemu Sajuki na kuwasisitiza kuenzi yale yote mema aliyokuwa akifanya kipindi cha uhai wake na kuwamasisha Umoja na Mshikamano baina yao.
Bw. Ridhiwani Kikwete naye alichangia Shilingi 500,000/=  kwa ajili ya kufanikisha mazishi ya Mpendwa wetu Sajuki anayetarajiwa kuzikwa Kesho Ijumaa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam.
Bw. Ridhiwani Kikwete akimfariji mama mzazi wa Marehemu Sajuki alipofika nyumbani hapo kuhani msiba huo.
Mganga wa Jadi anayefahamika kwa jina la Dokta Manyaunyau (kushoto) sambamba na Msanii wa filamu nchini Cloud wakisikiliza mawaidha ya waheshimiwa wabunge (hawapo pichani).

No
MUDA
TUKIO
MHUSIKA
1
1:00-……..
Waombolezaji kuwasili nyumbani kwa marehemu
Kamati yya mapokezi na Itifaki
2
2:00-2:45
Kisomo cha wanaume
Wanafamilia

3
2:45-3:30
Mwili wa marehemu kuwasili nyumbani
Kamati ya mazishi na familia.

4
3:30- 5:00
Salamu za pole kutoka kwa viongozi, ndg na jamaa
Kamati ya Itifaki
5
5:00- 6:00
Sadaka ya chakula
Wote

6
6:00-6:15
Nasaha toka kwa viongozi wa dini
Mashekhe

7
6:15
Mwili kuondoka nyumbani kuelekea msikitini
Kamati ya itifaki, usafiri na mazishi.
8
6:15-6:30
Kisomo cha kinamama
Kinamama

9
6:30 – 7:30
Mwili kuwasili msikitini na swala ya kuswalia maiti
Kamati ya mazishi na wahusika wa msikiti
10
7:30……
Mazishi
Shekhe na watu wote.

11

 Shukrani za mazishi na mwisho.
Familia na viongozi wa dini

Imetolewa na kamati ya mazishi.
Ahsanteni kwa ushirikiano

Taarifa ambazo zimeridhiwa na maamuzi ya familia na ndugu wa karibu, zinasema marehemu Juma Kilowoko aka Sajuki atazikwa siku ya ijumaa katika makaburi ya Kisutu.

Taarifa ambazo pia zimetoka kwa msemaji wa Bongo Movie na wahusika wa maandalizi ya mazishi hayo, wanasema ndugu wa Sajuki wameridhia marehemu kuzikwa hapa na sio Songea kama wengine wanavyotangaza. Kuhusu kusogeza mpaka ijumaa, msemaji huyo akasema, ni kutokana na kusubiri ndugu wa marehemu wanaotoka sehemu mbali mbali kuja Dar kwa ajili ya mazishi hayo, wengi wakitokea Songea.

Sajuki ambae alifariki usiku wa kuamkia tarehe 2, atazikwa siku ya ijumaa ya tarehe 4 katika makaburi ya Kisutu, ambapo mazishi hayo yataanza muda wa saa 5 asubuhi.

Mungu ailaze roho ya marehemu Juma Kilowoko (Sajuki) mahala pema peponi, Amen.

Face off: Mario Balotelli and Roberto Mancini (right) squared off in training

Leo asubuhi kumetokea hali ya kutokuelewana kati ya kocha Roberto Mancini na mchezaji toto tundu Mario Balotelli kiasi cha kufikia kushikana mashati na kutaka kupigana kama isingekuwa kuamuriwa na wachezaji wengine. Chanzo cha ugomvi wa wawili hao kinasemekana ni rafu ya Balotelli aliyomchezea mchezaji Scot Sinclair katika mazoezi hayo ya kujiandaa na mechi ya FA Cup dhidi ya Watford.
 
Altercation
The manager and player grapple with each other
Push and pull: Mancini and Balotelli raged at each other

Anger: Mancini was furious after a mistimed tackle from Balotelli 
Led off: The striker was pulled away from Mancini by a coach

 

No comments:

Post a Comment