Saturday, May 4, 2013

dogo alikuwa akipiga chabo katika tamasha la standard fm lililo fanyika wilaya ya ikungi.

Monday, January 21, 2013

KOMBE LA MATAIFA YA AFRIKA 2013



                  
        Seydou Keita Keita baada ya kufunga bao lake la kwanza dhidi ya Niger

Mali inayopewa nafasi ya kusonga katika hatua ya makundi, ya michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika, mwaka huu, imeandikisha ushindi wake wa kwanza katika mechi yake ya ufunguzi dhidi ya Niger.
Mali iliilaza Niger bao moja kwa bila katika mechi hiyo ya pili ya kundi B.
Seydou Keita, nahodha wa timu ya Mali, alifunga bao hilo la ushindi katika dakika ya 84 baada ya mlinda mlango wa Niger, Daouda Kassaly, kuutema mpira wa adhabu na kumfikia mfungaji.
Kwa matokeo hayo Mali, sasa inaongoza kundi B ikiwa na pointi tatu na goli moja.
Timu za DRC na Ghana zinafuatia katika msimamo wa kundi B, zikiwa na pointi moja kila moja baada ya timu hizo mbili kutoshana nguvu ya kufunga magoli mawili kwa mawili.
Hapo kesho mechi za kundi C, zinaanza huku mabingwa watetezi Zambia wakimenyana na Ethiopia, nayo Nigeria ikivaana na Burkina Faso.


 
                                                          Didier Drogba Noadha wa Ivory Coast

MANJI NA YANGA


Add caption

  Kocha mpya wa timu ya Yanga,kutoka nchini Uholanzi Ernest Brandts nae aliruhusiwa kutoa yake machache kuhusina na timu yake ya Yanga.     

Sunday, January 20, 2013

NDIKUMANA KUZIBA PEMGO LA NGASSA SUDAN

 
Suleiman Ndikumana akikaribishwa katika klabu yake mpya, El Merreikh ya Sudan ambayo imenunua baada ya Mrisho Ngassa wa Simba SC kukataa nafasi hiyo. Merreikh ilikuwa tayari kumnunua Ngassa kwa dola za Kimarekani 150,000 (zaidi ya Sh Milioni 230) ambazo zingelipwa kwa klabu zake, Simba SC anakocheza kwa mkopo kutoka Azam FC. Yeye mwenyewe angelipwa dau la dola 100,000 (zaidi ya Sh Milioni 150) la kusaini na mshahara wa dola 5,000 (zaidi ya Sh. Milioni 7.5). Lakini aliitema ofa huyo na anaendelea na mshahara wa Milioni 2, kwa mwezi Simba SC. Picha kwa hisani ya Ndikumana mwenyewe.
                              Ndikumana wa nne kutoka kulia akiwa na kikosi cha Merreikh

 Saviour: Clint Dempsey struck deep into injury-time to rescue a point for Spurs
              Saviour: Clint Dempsey struck deep into injury-time to rescue a point for Spurs
 
 
Saviour: Clint Dempsey struck deep into injury-time to rescue a point for Spurs
 
 
Breakthrough? Andreson (left), Patrice Evra (right) and Nick Powell (behind) were also wearing the night wear
Breakthrough? Andreson (left), Patrice Evra (right) and Nick Powell (behind) were also wearing the night wear.
 
Chilling with Bugs: Robin Van Persie (left) and Alexander Buttner (right) lounge in their Bugs Bunny pjs on the flight to Qatar
Chilling with Bugs: Robin Van Persie (left) and Alexander Buttner (right) lounge in their Bugs Bunny pjs en route for a team-building trip in Qatar
When in Doha, the team are planning to focus on team-building exercises at the $1.3billion Aspire Academy.
 
 

Thursday, January 17, 2013

WABABA WA BSS NDANI YA MKASA

mapozzz na kadenti


inadaiwa mapenzi yao yalianza kitambo wakati binti huyo akiwa kidato cha tatu lakini wakati huo pemzi lao lilikuwa la kawaida tu, kwani wababa alikuwa bado hajawa super star na hakuwa vizuri kifetha na heshima kwa jamii ilikuwa bado haimjui wababa. lakini mara tu baada ya kuchukua kifuta jasho cha bss na kupata wadau kibao wa muziki wa bongo flaver na show kadhaa hivyo kuwa na kiburi akampa mimba denti huyo ambaye aligundulika na wazazi lakini wao walitoa ujauzito huo (mimba). wazazi wa binti huyo walipata taalifa kuwa binti yao ametoa mimba na wababa alikamatwa na polisi na kuwekwa ndani kwa muda wa siku mbili. mpaka sasa kesi inaendelea huku wazazi wakiapa kumfunga wababa wakati huo huo binti huyo ametoweka na mpaka sasa ajulikani alipo.

 
unique sisters waja na new track 2013 "club banger"

Monday, January 14, 2013

NIMEKAMILISHA AJENDA ZANGU, NAWAACHIA SOKA SAFI NA YA KISTAARABU

Tenga akizungumza leo TFF

Na Boniface Wambura, Dar es Salaam
RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodegar Tenga amesema kwamba amekamilisha ajenda yake ya kulijenga shirikisho hilo kuwa taasisi, kwa kuweka mifumo bora ya uendeshaji ikiwemo kutengeneza katiba mpya na kanuni, hivyo hatagombea tena wadhifa huo katika uchaguzi uliopangwa kufanyika Februari 24 mwaka huu.
 
Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye ofisi za TFF leo, Rais Tenga amesema wakati anaingia kwenye uongozi mwaka 2004 ajenda ilikuwa na kuijenga TFF kama taasisi kwa kuweka mifumo ya uendeshaji ikiwemo kutengeneza katiba na kanuni, jambo ambalo limefanyika.
 
“Wajumbe wamekuwa wakiniuliza Rais vipi? Mimi hapana. Nilishafika pale pa kufika. Tulipoanza wakati ule ilikuwa ni kujenga taasisi. Na kazi hiyo tumeifanya. Tulipoingia mwaka 2004 hiyo ndiyo ilikuwa ajenda,” amesema Rais Tenga.
Amesema walitengeneza Katiba, vyombo huru vya kufanya uamuzi, kuongeza wigo wa wapiga kura ambapo hivi sasa kwenye mpira wa miguu hakuwezi kutokea migogoro, hata ikitokea kuna mfumo wa kuidhibiti.
 
Rais Tenga ameishukuru Sekretarieti ya TFF, Kamati ya Uchaguzi ya TFF, kamati za uchaguzi za wanachama wa TFF na vyama wanachama wa TFF kwa hatua iliyofikiwa katika uchaguzi ambapo mikoa yote imekamilisha uchaguzi na kubaki vyama shiriki pekee.
Ametoa mwito kwa wadau kujitokeza kugombea uongozi TFF, kwani baada ya kujenga taasisi ajenda iliyobaki ni mpira wa miguu wenyewe ikiwemo nini kifanyika ili mpira uchezwe katika maeneo mbalimbali.
 
“Tumeshatengeza mfumo, sasa ni kuangalia jinsi ya kuendeleza mpira. Changamoto ni tufanye nini ili mpira uendelee. Tunataka watu wengine wabebe hiyo ajenda ili tuangalie tunakwendaje mbele,” amesema.
Pia amesema ushirikiano ambao amepata kwa wapenzi na wadau wa mpira wa miguu ni wa ajabu. Vilevile ameishukuru vyombo vya habari, Serikali, klabu, wadhamini na wafadhili kwa mchango wao katika uendeshaji wa mpira wa miguu nchini.
Wakati huo huo, wadau 19 wamechukua fomu kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu.
 
Fomu hizo zimeanza kutolewa leo (Januari 14 mwaka huu) ambapo wawili wamechukua nafasi ya Makamu wa Rais wakati waliobaki wanaomba ujumbe wa Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda mbalimbali.
Waliochukua fomu za umakamu wa rais ni Wallace Karia na Ramadhan Nassib. Wote ni wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF inayomaliza muda wake.
 
Waliochukua fomu za Ujumbe ni Shaffih Dauda, Athuman Kambi, Hussein Mwamba, Stewart Masima, Yusuph Kitumbo, Mugisha Galibona, Vedastus Lufano, Twahili Njoki, Charles Mugondo, Elley Mbise, Farid Nahdi, Ayubu Nyaulingo, Nazarius Kilungeja, Epaphra Swai, Khalid Abdallah, James Mhagama na Selemani Bandiho. 
Katika hatua nyingine, TFF imeupongeza uongozi mpya wa Chama cha Soka Katavi (KAREFA) uliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika jana (Januari 13 mwaka huu).
Ushindi waliopata viongozi waliochaguliwa kuongoza chama hicho unaonesha jinsi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa KAREFA walivyo na imani kubwa kwao katika kusimamia mchezo huo mkoani Katavi.
 
TFF imeahidi kuendeleza ushirikiano wake kwa Kamati ya Utendaji ya KAREFA chini ya ukatibu wa Peter Hella aliyeibuka mshindi katika uchaguzi huo uliofanyika ukumbi wa DC mjini Mpanda kwa kumshinda Emmanuel Chaula kwa kura sita dhidi ya mbili.
 
TFF imesema uongozi huo mpya una changamoto nyingi, kubwa ikiwa ni kuhakikisha unaendesha shughuli za mpira wa miguu mkoani Katavi kwa kuzingatia katiba ya KAREFA pamoja na vyombo vya mpira wa miguu vilivyo juu yake.
TFF pia tunatoa pongezi kwa Kamati ya Uchaguzi ya KAREFA na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kwa kuhakikisha uchaguzi huo unaendeshwa kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za Wanachama wa TFF.
 
Viongozi waliochaguliwa ni Hella (Katibu), Elias Mande (Mjumbe wa Mkutano Mkuu TFF) na Deo Bakuba (Mwakilishi wa Klabu TFF). Nafasi ya Mwenyekiti haikuwa na mgombea wakati Mawazo Maso aliyekuwa mgombea pekee wa nafasi ya Makamu Mwenyekiti alipata kura nyingi za hapana. Nafasi zilizo wazi zitajazwa katika uchaguzi mdogo.
(Boniface Wambura ni Ofisa Habari wa TFF)

Baada ya kushuka mascut oman ngassa na wenzake


 

Sunday, January 13, 2013

MAN U AND LIVER

Me again: Robin van Persie scored the opener at Old Trafford to put United 1-0 up
Me again: Robin van Persie scored the opener at Old Trafford to put United 1-0 up
Lethal: Van Persie celebrated his 17th goal of the Premier League season
Lethal: Van Persie celebrated his 17th goal of the Premier League season
.
Battle: Danny Welbeck tries to hold off Martin Skrtel (right) of Liverpool
Battle: Danny Welbeck tries to hold off Martin Skrtel (right) of Liverpool
Keeping up appearances: Jose Mourinho (right) and Roy Hodgson (left) were at Old Trafford for the match
Keeping up appearances: Jose Mourinho (right) and Roy Hodgson (left) were at Old Trafford for the match
.
Recovery: Steven Gerrard had to make a last-ditch challenge on Van Persie after giving the ball away
Recovery: Steven Gerrard had to make a last-ditch challenge on Van Persie after giving the ball away
.
Audacious: Van Persie almost put United 2-0 up with this cheeky flick
Audacious: Van Persie almost put United 2-0 up with this cheeky flick
Ok? Pepe Reina was helped by Martin Skrtel after running into Shinji Kagawa
Ok? Pepe Reina was helped by Martin Skrtel after running into Shinji Kagawa
.
Red mist: Liverpool fans set off a flair during the match
Locking horns: Sir Alex Ferguson sought to guide United to another win over Liverpool at Old Trafford
Locking horns: Sir Alex Ferguson sought to guide United to another win over Liverpool at Old Trafford
Young pretender: Brendan Rodgers attempted to topple Liverpool's fierce rivals United in their own back yard
Young pretender: Brendan Rodgers attempted to topple Liverpool's fierce rivals United in their own back yard

Saturday, January 12, 2013

YANGA YAMALIZA MAZOEZI NCHINI UTURUKI


         


Wachezaji wa Young Africans, Juma Abdul, Said Bahanuzi & Didier wakifanya mazoezi ya Gym leo asubuhi katika Hotel ya Fame Residence


 Young Africans leo asubuhi imemaliza mazoezi  yake kwa kufanya mazoezi ya kujenga mwili na uimara (Gym) iliyopo katika hoteli ya Fame Residence leo asubuhi na yakiwa ndio mazoezi ya mwisho katika kambi ya mafunzo ya wiki mbili iliyokuwa ikiendelea katika viwanja vya Fame Residence Football mijini Antlaya.



Kocha mkuu Ernest Brandts akishirikiana na Fred Felix Mizniro na Razaki Siwa leo waliongoza mazoezi ya Gym kuanzia majira ya saa tatu na nusu asubuhi mpaka majira ya saa saa tano na nusu asubuhi ambapo baada ya mazoezi hayo wachezaji wamepewa nafasi ya kupumzika kujiandaa na safari ya hapo kesho kurudi Tanzania.
           
          KOCHA MFARANSA PATRICK LIEWING AANZA KAZI OMANA




Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig

Na Doris Maliyaga, Muscat
HII Simba bwana wacha tu. Imetia Oman ikiwa na wachezaji wanane lakini kama imekamilika na inaendelea na taratibu zake kama kawaida, huku kocha akiwataka wachezaji kucheza mchezo wa haraka haraka. 
Kocha Mkuu wa Simba, Mfaransa Patrick Liewig ili kutimiza azma yake amehakikisha anaongeza stamina kwa nyota wake. 
Mfaransa huyo amekuwa akiwatawanya wachezaji uwanja mzima mazoezini pamoja na ukweli kuwa wachezaji ni wachache. 
Kutokana na wachezaji hao kuhaha uwanja mzima, kwa kiasi kikubwa inawasaidia kuongeza pumzi. 

 
Liewig amesisitiza kuwa malengo yake ni kuona timu ikicheza mchezo wa pasi na kasi mithili ya Barcelona ya Hispania. 
Katika mazoezi ana wachezaji saba ambao ni Felix Sunzu, Haruna Moshi 'Boban', Haruna Shamte, Ramadhani Chombo 'Redondo', Kigi Makassy, Salim Kinje na Nassor Said 'Cholo'. 
Kipa Abel Dhaira kutoka Uganda alikuwa na tatizo la ngozi lakini amepona na anatarajiwa kuanza mazoezi leo Jumamosi. 
Dhaira inadawa alikuwa hawezi kuvaa viatu vya kuchezea kutokana na tatizo hilo. 


 
Akizungumza na Mwanaspoti daktari wa timu, Cosmas Kapinga alisema: "Kutokana na maendeleo yake tunatarajia kesho (leo Jumamosi) ataanza mazoezi na wenzake." 
Akizungumzia tatizo hilo, Dhaira alisema:"Tatizo hili linaninyima raha kwani malengo yangu ni kucheza mpira na si kukaa nje." 
Tatizo hilo inadaiwa lilitokea kutokana na kuchanganya hali ya hewa sehemu tofauti Iceland, Uganda, Tanzania na Oman.

Mazoezi ya Liewig
Mfaransa huyo anapenda kuona timu yake ikicheza kwa nafasi huku ikishambulia na kuzuia.
Liewig pia anasisitiza pasi bila kubutua na mpira lazima uanzishwe kutoka nyuma kwenda mbele. 
Pia ameweka mkazo katika kuhakikisha kuwa wacheza wanafanya vitendo kwa umakini. 
"Kila mmoja anapaswa kuwa makini na majukumu yake ya uwanjani." 
Kutokana na kutawanya nyota wake uwanja mzima, kumesaidia kuwasoma na bila shaka wanakuwa fiti zaidi. 
Timu hiyo jana Ijumaa asubuhi ilifanya mazoezi katika Uwanja wa Seeb. 
Katika mazoezi ya jioni walifanyia katika uwanja unaomilikiwa na Klabu ya Fanja. 
Wachezaji wengi wa Tanzania wamewahi kuchezea Fanja kama Ahmed Amasha, Yussuf Abeid, Talib Hilal, Hilal Hemed, Jamhuri Kihwelo, Abdulwakati Juma, Zahoro Salum, Innocent Haule, Madaraka Selemani na wengineo. 

Ilipojichimbia Simba
Simba ipo katikati ya mji wa Muscat, Oman katika hoteli ya kifahari ya Al Madinah Holiday kwani kambi ya awali pembezoni mwa fukwe za bahari imebadilishwa. 
Katika hoteli hiyo kuna kila kitu kinachohitajika kwa ajili ya mazoezi kwa wachezaji na mambo mengine, ina bwawa la kuogelea pamoja na gym ya mazoezi. 

 
Umbali kutoka Uwanja wa Ndege wa Muscat hadi ilipo hoteli hiyo ni dakika 15 kwa usafiri wa gari. 
Lakini pia kutoka katika hoteli hadi uwanja wa mazoezi wa Seeb ni kama dakika 18 kwa gari. Uwanja huo unamilikiwa na Shirikisho la Soka la Oman. 
Hali ya hewa 
Hali ya hewa ya hapa imetulia kabisa na haina tofauti kubwa na Tanzania kwani ni nyuzi joto 28. Kuna jua kwa mbali na baridi kidogo wakati wa jioni.

Wachezaji wengine
Simba imekuja kwa mafungu Oman, kwani wachezaji wengine walibaki kwa ajili ya Kombe la Mapinduzi na wengine walikuwa na kikosi cha Taifa Stars huko Ethiopia. 
Wachezaji waliobaki kwenye Kombe la Mapinduzi walitazamiwa kuwasili jana Ijumaa usiku wakiwa na Makamu Mwenyekiti, Geofrey Nyange 'Kaburu'. Wachezaji waliokuwa Stars, Juma Kaseja, Amir Maftah, Shomari Kapombe, Mrisho Ngassa, Amri Kiemba na Mwinyi Kazimoto walikuwa wanapaswa kuungana na kikosi hicho baada ya mechi ya jana kati ya Stars na Ethiopia huko Addis Ababa


 

 Na wakati  EMMANUEL Okwi na Mrisho Ngassa 'Anko' wameipotezea Simba nafasi ya kujipima na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo. Simba walipangiwa kucheza na Congo waliopiga kambi hapa kujiandaa na fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, mwaka huu. Mechi hiyo ilitakiwa kuchezwa leo Jumamosi. 
 
Kocha wa Simba, Patrick Liewig alifuta mchezo huo kutokana na kuwa na wachezaji wachache. 
Okwi anayeingarisha simba kutokana na kiwango chake, tangu alipokwenda kwao kwa mapumziko na kucheza mashindano ya Chalenji hajaripoti kambini na sasa imeripotiwa yupo Tunisia akifanya majaribio na klabu ya Esperance. 

 
Ngassa pamoja na Amir Maftah, Juma Kaseja, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto na Shomari Kapombe wako na Taifa Stars huko Ethiopia. 
Kocha wa zamani wa Simba, Talib Hilal, ambaye ni mwenyeji wao hapa, alisema Congo, ambayo inaongozwa na nahodha wake, Tresor Mputu walitaka mechi hiyo leo Jumamosi. 

 
Hata hivyo, Simba ina wachezaji wanane tu hapa; Felix Sunzu, Abel Dhaira, Nassor Said 'Cholo', Haruna Shamte, Kigi Makassy, Salim Kinje, Haruna Moshi 'Boban' na Ramadhani Chombo 'Redondo'. 
Wachezaji wengine walibaki Zanzibar kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi kabla ya kuondolewa hatua ya nusu fainali na Azam FC. 
Simba watacheza mechi ya kwanza dhidi ya timu ya Olimpiki ya Oman, Jumanne ijayo. Watajipima ubavu na Suwqi Januari 18 na watamaliza na Fanja FC.







JANGWANI WALUDI JE KUNAMPYA AU




Kikosi cha Young Africans kilichoanza kikiwa na kocha mkuu Ernest Brandts kabla ya kuanza kwa mchezo dhidi ya Emmen FC


Wachezaji wa Young Africans wakisalimiana na wachezaji wa Emmen FC kabla ya kuanza kwa mchezo
Young Africans imepoteza mchezo wake wa mwisho wa  kirafiki dhidi ya timu ya timu ya Emmen FC ya ligi daraja la kwanza nchini Uholanzi baada ya kufungwa kwa mabo 2-0 katika mchezo uliofanyika katika mji wa Bereke kwenye viwanja vya Arcuda foootball Antalya. 

Young Africans ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na kutengeneza nafasi za kufunga lakini kutokua makini kwa washambuliaji wake Nizar Khalfani, George Banda na Saimon Msuva kuliinyima Yanga kupata bao katika dakika 15 za kwanza,
 
Dakika ya 23 Saimon Msuva alishindwa kuipatia Yanga bao baada ya kushindwa kumalizia pasi safi nzuri ya Nizar Khalfani ambapo Msuva aliupiga mpira na kuokukolewa na mlinda mlango wa timu ya Emmen FC.
 
George Banda ambaye leo alianza kama mshambuliaji wa kati akisaidiana na Nizar Khalfani alishindwa pia kuipatia Yanga bao baada ya kushindwa kumalizia mpira uliopigwa na Haruna Niyonzima akitokea upande wa kushoto wa uwanja.
 
Mlinda mlango wa Yanga Said Mohamed alifanya kazi ya ziada kuokoa mipira miwili ya hatari langoni mwake baada ya washambuliaji wa Emmen kugongeana vizuri na kuwatoka walinzi wa Yanga lakini mashuti yao walikuta yakiishia mikononi mwake. 
 
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, Young Africans 0 - 0 Emmen FC.

Kipindi cha pili kilianza kwa Yanga kufanya mabadiliko ya kikosi chote ambapo waliingia, Yusuph Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ladslaus Mbogo, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Godfrey Taita, Omgea Seme, Didier Kavumbagu, Jerson Tegete na David Luhende.
 
Yanga ilianza tena mchezo kwa utulivu huku ikipanga mbinu za kuweza kupata bao la mapema lakini umakini wa walinzi wa Emmen Fc ulikuwa kikwazo kwa washambuliaji wa Yanga kuweza kuipita ngome hiyo.
 
Emmen FC waliitawala zaidi sehemu ya kiungo hali iliyopelekea kufanya mashambulizi mengi langoni mwa timu ya Yanga, na katika dakika ya 73 waliweza kujipatia bao la kwanza baada ya mfungaji kumalizia krosi iliyowapita walinzi wa Yanga.

Dakika nne (4) baadae, Emmen FC walijiapati bao la pili ikiwa ni dakika ya 77 baada ya mpira wa adhabu uliopigwa na kiungo wa Emmen FC kumponyoka mlinda mlango Yusuph Abdul na kugonga mwamba wa juu kabla ya mshambuliaji wa Emmen FC haujaukwmishwa wavuni na kuhesabu bao la pili.
 
Jerson Tegete aliumia dakika ya 79 katika harakati za kfunga na nafasi yake kuchukuliwa na Rehani Kibingu laikini mabadiliko hayo hayakuisadia Yanga kubadilisha matokeo.
 
Mpaka dakika 90 zinamalizika Young Africans 0 - 2 Emmen FC.
 
Mara baada ya mchezo kocha mkuu Ernest Brandts alisema amesikitishwa na matokeo hayo, timu yangu ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na kuwabana vizuri wapinzani wetu lakini kipindi cha pili umakini ulikosekana hali iliyopelekea kufungwa mabao mawili ya haraka haraka.
 
Makosa yaliyojitokeza katika kipindi cha pili tumeyaona kwa pamoja na benchi zima la ufundi hivyo tutayafanyia kazi yasijitokeze tena katika michezo itakayofuata alisema 'Brandts' .
 
Yanga kesho itafanya mazoezi ya mwisho asubuhi kabla ya kuanza kujiandaa na safari ya nchini Tanzania siku ya jumapili mchana ambapo itarajiwa kufika Dar es salaam majira ya saa 10 kasoro ikiwa ni siku ya jumatatu alfajiri.
 
Kikosi kilichoanza kipindi cha kwanza: Said Mohamed, Juma Abdul, Stephano Mwasika,  Nadir Haroub 'Cannavaro', Shadrack Nsajigwa, Nurdin Bakari, Saimon Msuva, Frank Domayo, Geroge Banda, Nizar Khalfani,  Haruna Niyonzima
 
Kikosi cha kipindi cha pili: Yusuph Abdul, Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Ladislaus Mbogo, Kelvin Yondani, Athuman Idd 'Chuji, Godfrey Taita, Omega Seme, Didier Kavumbagu, Jerson Tegete/Rehani Kibingu, David Luhende 




Na Boniface Wambura, Addis Ababa
TIMU ya soka ya ya taifa ya Tanzania, imepoteza mchezo wa kirafiki dhidi ya Ethiopia uliochezwa leo kwenye Uwanja wa Addis Ababa hapa mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Mechi hiyo iliyochezeshwa na Bamlak Tesema wa Ethiopia ilikuwa ya kusisimua, hasa kutokana na timu zote kucheza kwa kasi kwa muda wote. Wenyeji Ethiopia ndiyo walioanza kupata bao dakika ya 13 lililofungwa na Fuad Ibrahim akiwa wastani wa hatua sita kutoka kwa mlinda mlango Juma Kaseja wa Taifa Stars.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi kama kilivyokuwa cha kwanza, huku Ethiopia wakiwa wamefanya mabadiliko kwa wachezaji watano. Tanzania ilifanikiwa kusawazisha bao hilo dakika ya 50 likifungwa na Mbwana Samata baada ya kumzidi maarifa beki mmoja wa Ethiopia.
Bao la ushindi kwa Ethiopia lilifungwa kwa kichwa dakika ya 69 na mshambuliaji Shemelis Bekele aliyeingia kipindi cha pili akiunganisha mpira wa krosi uliopigwa na winga Yossuf Sallah kutoka upande wa kushoto.
Taifa Stars inarejea nyumbani kesho (Jumamosi, Januari 12 mwaka huu) ambapo itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 7 kamili mchana kwa ndege ya Ethiopian Airlines.
Taifa Stars: Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Amri Kiemba, Mrisho Ngasa, Salum Abubakar, Thomas Ulimwengu/Khamis Mcha, mwinyi Kazimoto na Mbwana Samata.

Haruna Moshi Boban akiwaongoza wachezaji wenzie wa Simba kwenye mazoezi ya leo asubuhi

Mazoezi ya viungo yakiendelea

Kocha wa Simba Patrick Leiwing akiongoza mazoezi leo asubuhi


Kiggy Makasi dimbani

PICHA ZOTE NA SALEH ALLY WA CHAMPIONI

Friday, January 11, 2013

LIVERPOOL NA MAN U

TRACK MPYA YA BELL 9 2013

Producer Tiddy Hotter wa studio ya One love fx amesema kuwa Bell 9 amesha maliza ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina la LISTEN  teyali ipo hewani.


SIMBA SC WAPAA OMAN LEO, WAACHA KIKOSI TISHIO MAPINDUZI

 

MABINGWA wa Bara, Simba SC wanatarajiwa kuondoka leo Dar es Salaam kwenda Oman kuweka kambi ya wiki mbili kujiandaa na Ligi Kuu pamoja na Ligi ya Mabingwa Afrika.  

Kuhusu Kombe la Mapinduzi, Simba imegawa vikosi viwili na kile ambacho kilichukua Kombe la Sup8R Banc ABC kwa kuzifunga Azam FC na Mtibwa Sugar ndicho kitabaki kwenye Kombe la Mapinduzi chini ya kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ na Mganda Richard Hamatre.

Kikosi hicho cha Mapinduzi kina wakali kama Ramadhan Singano ‘Messi’, Edward Christopher, Abdallah Seseme, Haruna Chanongo, Hassan Isihaka, Hassan Hatibu, Miraj Adam na wengine ambao wote wanachezea Simba A.

Wachezaji wanaobaki kwenye Kombe la Mapinduzi, watakwenda Oman baada ya mashindano hayo pamoja na kocha Julio.

Simba SC kesho inatarajiwa kumenyana na Azam FC katika Nusu Fainali ya Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Mchezo huo utakuwa ni marudio ya Nusu Fainali ya mwaka jana, ambayo Azam FC waliitoa Simba SC kwa kuichapa mabao 2-1.

Kocha Msaidizi wa Azam FC, Muingereza Kalimangonga Sam Daniel Ongala, maarufu kama Kali, amesema kwamba wamefurahia kukutana na Simba SC katika Nusu Fainali kuliko Tusker ya Kenya, kwa sababu hiyo itakuwa njia ya mkato kwao kuingia Fainali.

Ikiwa Oman, Simba itakaa kwa wiki mbili na itacheza mechi tatu za kujipima nguvu dhidi ya timu ambazo wameandaliwa na wenyeji wao Fanja FC. Aidha, wameandaliwa makocha watatu huko, wakiongozwa na beki wa zamani wa Simba SC, Talib Hilal kuungana na makocha wa Simba kuinoa klabu hiyo ikiwa nchini humo.
Hiyo ni ziara ya mafunzo, ambayo lengo lake ni kuiweka sawa Simba SC kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Bara na Ligi ya Mabingwa Afrika.