Seydou Keita Keita baada ya kufunga bao lake la kwanza dhidi ya Niger
Mali inayopewa nafasi ya kusonga katika hatua ya
makundi, ya michuano ya kuwania kombe la mataifa bingwa barani Afrika,
mwaka huu, imeandikisha ushindi wake wa kwanza katika mechi yake ya
ufunguzi dhidi ya Niger.
Mali iliilaza Niger bao moja kwa bila katika mechi hiyo ya pili ya kundi B.
Seydou Keita, nahodha wa timu ya Mali, alifunga
bao hilo la ushindi katika dakika ya 84 baada ya mlinda mlango wa Niger,
Daouda Kassaly, kuutema mpira wa adhabu na kumfikia mfungaji.
Kwa matokeo hayo Mali, sasa inaongoza kundi B ikiwa na pointi tatu na goli moja.
Timu za DRC na Ghana zinafuatia katika msimamo
wa kundi B, zikiwa na pointi moja kila moja baada ya timu hizo mbili
kutoshana nguvu ya kufunga magoli mawili kwa mawili.
Hapo kesho mechi za kundi C, zinaanza huku
mabingwa watetezi Zambia wakimenyana na Ethiopia, nayo Nigeria ikivaana
na Burkina Faso.
Didier Drogba Noadha wa Ivory Coast